Kipa Joe Hart kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu West Ham

Joe Hart Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kipa Joe Hart alikaa msimu uliopita Torino kwa mkopo na kuchezea klabu hiyo ya Italia mechi 36

Mlinda lango wa England Joe Hart amepangiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu leo Jumatatu kabla ya kutia saini mkataba wa kukaa West Ham msimu mmoja kwa mkapo.

Hart alikuwa ameambiwa na meneja wa Manchester City Pep Guardiola ajitafutie klabu nyingine baada yake kukaa msimu uliopita Torino.

Inatarajiwa kwamba City watakuwa wakilipa sehemu ya ujira wake.

Mkataba huo unatarajiwa kuwa na kifungu ambapo West Ham wanaweza kuruhusiwa kumnunua kabisa mchezaji huyo wa miaka 30.

Mkataba wa Hart katika Manchester City utafikia kikomo 2019.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii