Clinton Njie njiani kuelekea Marseille

Clinton Njie celebrates scoring for Marseille Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Clinton Njie alifunga mabao manne akiwa na Marseille kwa mkopo msimu uliopita

Mshambuliaji wa Tottenham Clinton Njie anatarajiwa kujiunga na klabu ya Marseille ya Ufaransa kwa mkataba wa kudumu baada ya klabu hizo kuafikiana.

Raia huyo wa Cameroon wa umri wa miaka 23 alikuwa klabu hiyo ya Ligue 1 kwa mkopo msimu uliopita, ambapo alifunga mabao manne.

Njie alijiunga na Spurs kutoka Lyon mwaka 2015 kwa £10m na kuchezea klabu hiyo mechi 14, ingawa aliumia kwenye goti Desemba 2015.

"Tunamtakia Clinton kila la kheri siku zake za baadaye," Tottenham wamesema.

Mada zinazohusiana