Diego Costa avalia jezi ya Atletico Madrid

Diego Costa

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uhispania, Diego Costa amepiga picha za video akifurahia likizo yake huku akiwa amevalia jezi ya Atletico Madrid.

Mustakabali wa Costa bado haujawekwa sawa toka nyota huyo alipobainisha kuwa Conte alimwambia kuwa hahitajiki tena kwenye klabu hiyo.

Matokeo hayo yamemfanya Costa mwenye umri wa miaka 28 kuachwa katika kikosi cha Chelsea kilichoanza maandalizi ya msimu ujao huku kukiwa na matumaini ya kupata klabu mpya.

Mada zinazohusiana