Wakaso atua Alaves, West Brom yamsajili Hegazi

Wakaso Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mubarak Wakaso

Mchezaji wa kimataifa wa Ghana Mubarak Wakaso amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na klabu ya Alaves ya nchini Hispania.

Mchezaji huyu amejiunga na timu hiyo akitokea Panathinaiko ya Ugiriki, Wakaso anauzoefu wa ligi ya Hispania la Liga, ambapo aliwahi kuvichezea vilabu vya Granada, Las Palmas, Espanyol, Villareal na Elche.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ahmed Hegazi (kulia) alipokua akiichezea Fiorentina ya Italia

Nayo klabu ya West Bromwich Albion ya nchini England, imemsajili beki wa Misri Ahmed Hegazi kwa mkopo akitokea klabu ya Al Ahly.

Hegazi alirejea nyumbani kwao Misri na kujiunga na Al Ahly mwaka 2015, baada ya kuondoka katika klabu ya Fiorentina kwa kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.