Man United yaichapa Real Salt

Lukaku Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshambuliaji mpya Man United Romelu Lukaku mfungaji wa bao la ushindi katika mchezo dhidi ya Real Salt Lake

Timu ya Manchester United imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya Real Salt Lake katika mchezo wa kirafiki uliofanyika huko nchini Marekani. mabao ya timu hiyo yalifungwa na Henrikh Mkhitaryan na Romelu Lukaku huku goli la Real Salt Lake likifungwa na Luis Silva.

Wahispania wa Sevilla imeichapa Cerezo Osaka ya Japan kwa mabao 3-1,Wolfsburg wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Hansa Rostock

Sturm Graz na West Ham United wametoshana nguvu kwa sare ya bila kufungana .Real Union wamelala kwa kufungwa 3-1na Eibar.

Athletic Bilbao nao Fenerbahce nao wametoshana nguvu kwa mchezo kumalizika kwa sare ya bila bila.