Caf yatathmini kubadili tarehe ya kuandaa kombe la taifa bingwa Afrika

Confederation of African Football president Ahmad Haki miliki ya picha Cafonline
Image caption Caf yatathmini kubadili tarehe ya kuandaa kombe la taifa bingwa Afrika

Kombe la taifa bingwa barani Afrika huenda likahamishwa hadi msimu wa joto kama sehemu ya mazungumzo yaa shirikisho la kandanda barani Afrika.

Kuandaliwa mashindano hayo miezi ya Januari na Februari imeghadhabisha vilabu vya bara Ulaya ambapo wachezaji wengi wa kiafrika hucheza.

Pia idadi ya timu zinashoriki huenda ikaongezwa kutoka 16 hadi 24.

Wachezaji wengine walikataa ombia la kuwataka kujiunga nchi zao kushirikia mashindani ya mwaka huu, yaliyoandaliwa nchini Gabon na kuamua kubaki na vilabu vyao.

Haki miliki ya picha ISSOUF SANOGO
Image caption Hao ni pamoja na wachezaji kadha kutoka Cameroon ambao walitaka kujiunga na timu ambayo hata hivyo ilishinda kombe hilo.

Hao ni pamoja na wachezaji kadha kutoka Cameroon ambao walitaka kujiunga na timu ambayo hata hivyo ilishinda kombe hilo.

Kila baada ya miaka miwoli mzo huibuka kati ya vilabu vya Ulaya na nchi, vinavyodai kuwapoteza wachezaji wakati wanahitaji sana.

Kwa mujibu wa vilabu hivyo mara nyingi wachezaji hurudi vilabuni wakati wamechoka baada ya kuishiriki mechi za taifa bingwa barani Afrika.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii