Hart,Lucas wakamilisha usajili wao

Hart Joe Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Joe Hart

Golikipa Joe Hart amekamilisha usajili wa kujiunga na West Ham United, kwa mkopo wa muda mrefu akitokea Manchester City.

Hart msimu uliopita alicheza kwa mkopo katika klabu ya Torino, ya ligi kuu ya Italia, baada ya kocha wa Man City Pep Guardiola, kutokumpa nafasi na kumtoa kwa mkopo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Lucas Leiva akiwa kavaa jezi ya timu yake mpya

Nae kiungo Lucas Leiva amekamilisha uhamisho wake kuijiunga na Lazio kwa dau la pauni 5 akitokea Liverpool.

Nyota huyu raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 30 aliichezea Liverpool jumla ya michezo 345. toka aliposajiliwa na timu hiyo akitokea Gremio ya nchini kwao miaka 10 iliyopita.