Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 19.07.2017 na Salim Kikeke

Neymar Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Neymar anadaiwa kukubali kwenda PSG

Mshambuliaji wa Barcelona Neymar, 25, amekubali dau la Paris Saint-Germain, baada ya klabu hiyo ya Ufaransa kuwa tayari kutoa pauni milioni 195. (Esporte)

Makamu wa rais wa Barcelona Jordi Mestre amesisitiza kuwa Neymar hatoondoka Barcelona wakati wowote ule. (Star)

Mtaalam wa soka wa Amerika ya kusini Tim Vickery amesema Neymar huenda akaondoka Barcelona ili kuepuka kuwa chini ya kivuli cha Lionel Messi. (BBC Radio 5 Live)

Kiungo wa Everton Ross Barkley, 23, anataka mshahara wa pauni 150,000 kwa wiki ili kujiunga na Tottenham, huku klabu yake ya Everton ikitaka pauni milioni 50 kama ada ya uhamisho. (Mirror)

Tottenham watalazimika kumlipa kiungo Moussa Sissoko, 27, ili aondoke, licha ya kutoa pauni milioni 30 kumsajili mwaka jana tu. (Daily Mail)

Arsenal watajaribu kutaka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzima, 29, iwapo Alexis Sanchez, 28, ataondoka Emirates. (Don Balon)

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema Alexis Sanchez, 28, anayesakwa na Manchester City, hauzwi. (Sky Sports)

Paris Saint-Germain wameibuka tena na lengo la kumtaka Alexis Sanchez, 28, na wana uwezekano mkubwa wa kumsajili. (Telegraph)

Haki miliki ya picha Empics
Image caption Alexis Sanchez

Wakala wa Alexis Sanchez amewapa Real Madrid nafasi ya kumsajili mchezaji huyo wa Arsenal, lakini Real wamekataa kumchukua mchezaji huyo wa zamani wa Barcelona. (OK Diario)

Newcastle na Crystal Palace wanafikiria kumchukua kipa wa West Ham Adrian, baada ya klabu yake kumsajili kwa mkopo Joe Hart kutoka Manchester City. (Mirror)

Swansea wamemuulizia mshambuliaji wa Manchester City Wilfried Bony, 28, aliyecheza kwa mkopo Stoke msimu uliopita. (Foot Mercato)

Ivan Perisic, 28, amesafiri na klabu yake kwenda China baada ya Manchester United kushindwa kufikia makubaliano ya ada ya uhamisho na Inter Milan. (Telegraph)

Manchester United wameacha kumfuatilia kiungo Eric Dier, 23,wa Tottenham baada ya klabu hiyo ya kaskazini mwa London kukataa kumuuza mchezaji huyo. (Mirror)

Image caption Wlifried Bonny

Manchester United wamekuwa na mazungumzo ya awali na Paris Saint-Germain kuhusu kutaka kumsajili Marco Verratti. United wapo tayari kupambana na Barcelona kutaka kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa Italy. (TuttoMercatoWeb)

Borussia Dortmund wameamua kutomuuza Pierre Emerick-Aubameyang, 28, baada ya mchezaji huyo kuhusishwa na kuhamia Chelsea kwa pauni milioni 70. (Kicker)

Chelsea hawataki kutoa euro milioni 30.8 wanazotaka Real Madrid kwa ajili ya beki wa kulia Danilo. (Evening Standard)

Beki wa Southampton Virgil van Dijk hajawasilisha maombi ya kuondoka kama njia ya kulazimisha uhamisho wake kwenda Liverpool. (Daily Echo)

Beki wa Barcelona Aleix Vidal amekataa nafasi ya kuhamia Juventus, kuziba pengo la Dani Alves aliyekwenda PSG. (Sport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Beki wa upande wa kulia wa Juventus Dani Alves anatarajiwa kwenda PSG

Arsenal wanakaribia kumsajili mshambuliaji kutoka Feyenoord Joshua Zirkzee, 16, aliyekuwa akinyatiwa na Ajax. (SoccerNews)

Jack Wilshere, 25, ameambiwa anaweza kuondoka Arsenal. (Mirror)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii (Kwa Kiingereza): Uhamisho wa wachezaji Ulaya

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na siku njema.

Mada zinazohusiana