Kipa wa Arsenal Wojciech Szczesny ahamia Juventus

Wojciech Szczesny Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wojciech Szczesny alikaa misimu miwili kwa mkono Roma

Kipa wa Arsenal kutoka Poland Wojciech Szczesny amehamia katika kalbu ya Juventus ya Italia kwa £10m.

Mlinda lango huyo wa miaka 27 alikaa miaka miwili iliyopita kwa mkopo katika klabu ya Roma.

Sasa, ametia saini mkataba wa kudumu wa miaka minne katika mabingwa wa Italia, Juventus.

Raia huyo wa Poland alichezea Roma mechi 38 msimu uliopita na kumaliza mechi 14 bila kufungwa, nyingi za mechi hizo zikiwa katika Serie A.

"Unapofika Juve, ni kwa sababu umeteuliwa. Sikukawia," anasema Szczesny, ambaye alichezea Arsenal mechi 132 katika kipindi cha miaka minane.

Szczesny atakuwa sasa anashindania lango na Gianluigi Buffon.

Juventus wamesema tayari wamezungumza na Buffon kuhusu hilo.

Mada zinazohusiana