Aguero hauzwi asema Guardiola

GUARDIOLA Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kocha wa Man City Pep Guardiola

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amethibitisha hana mpango wa kuuza mshambuliaji wake Sergio Aguero kun.

"Ni mchezaji wetu na atabakia hapa,"alisema Guardiola wakati akizungumzia tetesi za mchezaji huyo huenda akaondoka.

Hata hivyo kocha huyo amesema wanahitaji kusajili wachezaji wengine watatu au wanne katika kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao.

Man City imekua kwenye mawindo ya kuwania saini za walinzi Danilo wa Real Madrid na Benjamin Mendy anayekipiga na katika timu ya Monaco, pamoja na mshambuliaji hatari wa Arsenal Alexis Sanchez.