Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 20.07.2017 na Salim Kikeke

Diego Costa and Antonio Conte Haki miliki ya picha Getty Images

Paris Saint-Germain wanajiandaa kuzungumza na Barcelona kuhusu uhamisho wa pauni milioni 196 wa Neymar, 25. (Guardian)

PSG wapo tayari kumpa Neymar pauni milioni 45, za kukubali tu kujiunga nao, na mshahara wa pauni 596,000 kwa wiki (baada ya makato ya kodi) na mkataba wa miaka mitano. (Daily Mail)

Barcelona wanapanga kuzungumza na Monaco kuhusu kumsajili Kylian Mbappe, 18. Barca wanatarajia kupata fedha za kutosha kumsajili Mbappe baada ya kumuuza Neymar, 25. (Daily Mail)

Chelsea wanataka pauni milioni 44 kutoka kwa Atletico Madrid kwa ajili ya Diego Costa, 28, baada ya kukamilisha usajili wa Alvaro Morata, 24, kutoka Real Madrid. (Independent)

Rais wa Atletico Madrid Enrique Cerezo amesema hakuna uhakika thabiti iwapo Diego Costa atakwenda Atletico Madrid. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Neymar alihamia Barcelona mwaka 2013

Chelsea, Tottenham na Manchester United huenda zikaingia katika mapambano ya kumgombania kiungo wa Everton Ross Barkley, 23. (The Times)

Liverpool wapo tayari kutoa pauni milioni 70 kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, 22, baada ya dau la pauni milioni 66 kukataliwa. (Mirror)

West Ham wanakaribia kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier 'Chicharito' Hernandez, 29, kutoka Bayer Leverkusen. (Sky Sports)

Arsenal wamewaambia West Ham kuwa watalazimika kutoa pauni milioni 20 ikiwa wanamtaka kiungo Jack Wilshere, 25. (Daily Star)

Paris Saint-Germain wamemtuma mkurugenzi wao wa michezo kwenda London kujaribu kumshawishi Alexis Sanchez, 28, ambaye pia anasakwa na Manchester City. (Sun)

Everton wamepata matumaini zaidi ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud, 30. (The Telegraph)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Alexi Sanchez

Kiungo wa Arsenal Mohamed Elneny amekataa kuhamia Leicester City waliokuwa tayari kutoa pauni milioni 10 kumsajili. (The Sun)

Manchester City wanakaribia kumsajili beki wa Real Madrid Danilo, 26, kwa pauni milioni 26.5. (Guardian)

Manchester city wanakaribia kukamilisha usajili wa beki Benjamin Mendy, 23, kutoka Monaco. (Times)

Manchester United wanahusishwa na kutaka kumsajili kiungo wa Paris Saint-Germain, Marco Verratti, 24, baada ya mchezaji huyo kumfanya Mino Raiola kuwa wakala wake mpya. (Sun)

Image caption Anthony Martial kushoto na mkufunzi Jose Mourinho

Manchester United na Chelsea zilitazama uwezekano wa kumsajili Neymar, lakini timu hizo mbili zilikatishwa tamaa na bei ya pauni milioni 196 ya mchezaji huyo, 25, kutoka Brazil. (Independent)

Inter Milan wamewaambia Manchester United lazima wamjumuishe Anthony Martial, 21, katika mkataba wowote utakaohusu uhamisho wa Ivan Perisic, 28. (Independent)

AC Milan wamesema kiungo mshambuliaji wao Suso, 23, anayenyatiwa na Tottenham, hauzwi. (Tuttomercato)

PSG watamuuza kiungo Blaise Matuidi, 30, iwapo dau zuri litatolewa. (L'Equipe)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Blaise Matuidi

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii (Kwa Kiingereza): Uhamisho wa wachezaji Ulaya

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na siku njema.

Mada zinazohusiana