Mwana wa Pele ajisalimisha kwa maafisa polisi

Mwana wa Pele ajisalimisha kwa polisi ili kuendelea kuhudumia kifungo cha miaka 13 jela
Maelezo ya picha,

Mwana wa Pele ajisalimisha kwa polisi ili kuendelea kuhudumia kifungo cha miaka 13 jela

Mtoto wa kiume wa mwanasoka gwiji nchini Brazil Pele amejisalimisha kwa polisi na ataanza kutumikia kifungo cha miaka 13 jela kwa makosa yanayohusiana na biashara ya ulanguzi wa fedha na dawa za kulevya.

Edson Nascimento, kwa kifupi Edinho, pia alikuwa mlinda lango mashuhuri katika klabu ya soka ya baabaake Santos.

Lakini aligubikwa na sakata hiyo yapata miaka 12 iliyopita .

Awali alikuwa amepewa kifungo cha miaka 33 lakini kikapunguzwa baada ya kukata rufaa na katika kukwepa jela kwa mda wote huu hadi sasa ambapo amejisalimisha kuanza kutumikia kifungo kilichosalia cha miaka 13 gerezani.