Chelsea yaizaba Arsenal 3-0 mechi ya kirafiki

Michy Batschuayi aliisaidia Chelsea kuinyoa bila maji Arsenal
Maelezo ya picha,

Michy Batschuayi aliisaidia Chelsea kuinyoa bila maji Arsenal

Chelsea ilifanikiwa kulipiza kisasi na kujizolea sifa kufuatia kushindwa kwao katika kombe la FA miezi miwili iliopita baada ya Michy Batschuayi kuwasaidia vijana wa Antonio Conte kuicharaza Arsenal 3-0.

Mchezaji huyo wa Ubelgiji alimpigia pasi muruwa Willian katika dakika ya 40 kabla ya Chelsea kufunga dakika mbili baadaye.

Batshuayi baadaye alifunga bao jingine baada ya kipindi cha kwanza na kufanya mambo kuwa 3-0, matokeo ambayo yataipatia motisha kmubwa Chelsea wakati ambapo wanatarajiwa kuchuana na Bayern Munich na Inter Milan ya Itali.

Arsene Wenger hatahivyo atakuwa na wasiwasi mkubwa baada ya Chelsea kuishinda Arsenal kwa urahisi mkubwa.

Ilikuwa chini ya miezi miwili wakati Arsenal iliishinda Chelsea 2-1 katika fainali ya kombe la FA uwanjani Wembley katika mechi ambayo Arsenal ilionyesha mchezo wa hali ya juu.