David Ferrer ashinda taji la Swedish Open

Ferrer ameshinda taji hili mwaka 2007 na 2012
Maelezo ya picha,

Ferrer ameshinda taji hili mwaka 2007 na 2012

David Ferrer amemchapa Alexandr Dolgopolov na kufanikiwa kuwa bingwa wa michuano ya Swedish Open.

Hili ni kombe kubwa kwa Muispaniola huyo tokea ameshinda kikombe cha Vienna Open miaka miwili iliyopita.

Ferrer ameshinda kwa seti 6-4 6-4 na kupata taji la 27 kwenye historia yake katika mchezo uliokuwa na ushindani mkali.

Ferrer anashika nafasi ya 46 kwa ubora duniani.