Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 24.07.2017 na Salim Kikeke

Mshambuliaji wa Barcelona Neymar katikati, 25, amewaambia wachezaji wenzake, Lionel Messi na Luis Suarez, kuwa atabakia Barca
Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Barcelona Neymar katikati, 25, amewaambia wachezaji wenzake, Lionel Messi na Luis Suarez, kuwa atabakia Barca

Mshambuliaji wa Barcelona Neymar, 25, amewaambia wachezaji wenzake, Lionel Messi na Luis Suarez, kuwa atabakia Barca baada ya wawili hao kumshawishi kutojiunga na Paris Saint-Germain kwa uhamisho utakaovunja rekodi ya dunia wa pauni milioni 200. (Sport)

Cristiano Ronaldo amemtaka Neymar kutohamia PSG na kusubiri kwenda Manchester United wakati utakapowadia. (Diario Gol)

Meneja wa Inter Milan Luciano Spalletti ameionya Manchester United kwa kusema watoe pauni milioni 48 kama wanamtaka Ivan Perisic, vinginevyo wasahau kumsajili winga huyo. (The Sun)

Maelezo ya picha,

Alexis Sanchez

Arsene Wenger amedai kuwa PSG wanataka kumsajili Neymar kwa sababu wameshindwa kumsajili Alexis Sanchez. (Daily Mirror)

Monaco wamesema wanataka pauni milioni 55 kumuuza winga Thomas Lemar, 21, ambaye anasakwa na Arsenal. (Daily Star)

Manchester United wapo tayari kuwapa PSG pauni milioni 70 ili kumsajili kiungo Marco Verratti. (Daily Express)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Marco Verratti

Marco Verratti amesema chaguo lake la kwanza ni kwenda Barcelona, ingawa pia yuko tayari kwenda Manchester United. (Express)

Manchester United wapo tayari kupanda dau kumtaka kipa chipukizi wa Bolton Wanderers Jake Turner, 18. (The Sun)

Juventus wameacha kumfuatilia kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic, 28 na hivyo kutoa mwanya kwa Manchester United kukamilisha uhamisho wake. Chelsea wamesema wanataka pauni milioni 40 ambazo Juve hawapo tayari kutoa. (Telegraph)

Maelezo ya picha,

David de Gea

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ametoa "hakikisho la 100%" kwa mashabiki kuwa kipa David de Gea atakuwepo Old Trafford msimu huu mpya. (Telegraph)

Manchester United na Arsenal huenda wakapambana katika kumsajili winga wa Real Madrid Marco Asensio, 21. (Don Balon)

Deportivo la Coruna wamempa mkataba wa miaka kumi Lucas Perez katika jitihada za kumshawishi mshambuliaji huyo wa Arsenal kurejea katika klabu yake hiyo ya zamani. (DXT Campeon)

Mazungumzo ya uhamisho wa mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28 kwenda PSG yameporomoka kutokana na bei kubwa ya ada ya uhamisho na mshahara anaodai. (Le Parisien)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

William Carvalho

Arsenal wanajiandaa kupanda dau la takriban euro milioni 30 kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon William Carvalho. (Record)

Chelsea wataongeza bidii katika kutaka kumsajili kiungo wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 23, wiki hii ingawa huenda wakakabiliwa na ushindani kutoka Manchester City. (Express)

Chelsea wanataka kuwazidi kete Manchester United na AC Milan katika kumsajili mshambuliaji wa Fluminese Ricjardlison. (Gianluca Di Marzio)

Jurgen Klopp amesema kiungo wake Emre Can haendi popote. (Liverpool Echo)

Maelezo ya picha,

Virgil van Dujk

Liverpool wanasubiri kuona kama Southampton watakuwa tayari kuzungumzia uhamisho wa Virgil van Dujk. (Liverpool Echo)

West Brom wanajiandaa kutoa pauni milioni 10 kumsajili beki wa Manchester United Chris Smalling, 27. (Daily Star)

Matumaini ya Liverpool kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita yamefifia baada ya klabu hiyo kusisitiza kuwa haumuuzi mchezaji huyo. (Sky Sports)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na Jumatatu.