Eilidh Doyle kurudisha kumbukumbu za wakongwe Uingereza

Doyle amesema anapaswa juhudi kufikia rekodi za wakongwe hao
Maelezo ya picha,

Doyle amesema anapaswa juhudi kufikia rekodi za wakongwe hao

Eilidh Doyle anatarajiwa kurudisha kumbukumbu za wakimbiaji wa zamani Christine Ohuruogu na Dai Greene wakati atakapoiongoza timu ya taifa ya Uingereza ya riadha mjini London mwezi ujao.

Greene alikuwa mkimbiaji wa timu ya Uingereza katika michezo ya London 2012, huku Ohuruogu akiwa nahodha katika mbio za dunia za 2013 huku wote wakiweka rekodi za kuvutia.

Maelezo ya picha,

Christine Ohuruogu aliiongoza Uingereza katika mbio za dunia 2013

Doyle amesema atajaribu kufuata nyayo za wakimbiaji hao wenye historia nzuri licha ya kukiri kuwa sio jambo jepesi.

Maelezo ya picha,

Dai Green alikua nahodha wa Uingereza 2012

Ohuruogu alikuwa mwanamichezo wa kwanza wa kike wa Uingereza kuwa bingwa wa dunia mara mbili , akishinda pia medali ya dhahabu katika michuano ya mwaka 2009 mita 400 huko Berlin.