Chelsea na Alvaro Morata wapoteza kwa Bayern Munich

Mchezaji Alvaro Morata wa Chelsea akiwapita wachezaji wa Bayern Munich katika mechi iliokwisha 3-2

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mchezaji Alvaro Morata wa Chelsea akiwapita wachezaji wa Bayern Munich katika mechi iliokwisha 3-2

Mshambuliaji wa Chelsea Alvaro Morata alianza mechi yake ya kwanza kwa kutoa pasi iliosababisha bao katika mechi ambayo timu yake iliopoteza 3-2 dhidi ya Bayern Munich katika mechi ya kirafiki mjini Singapore.

Mshambuliaji huyo wa Uhispania aliyejiunga kwa uhamisho wa kitita cha pauni milioni 60 ulioweka rekodi ya klabu kutoka Real Madrid wiki iliopita aliingia katika kipindi cha pili.

Huku Chelsea ikiwa imefungwa bao 3-1, Alonso aliugusa mpira wa kona uliopigwa na Cesc Fabregas ili Michy Batshuayi kufunga.

Bao la Rafinha na mawili ya Thomas Muller yaliisaidia Bayern kuibuka washindi kabla ya Marcos Alonso kuifungia Chelsea.