Nyota wa mchezo wa raga Kenya auwawa

Mchezo wa raga nchini Kenya unaomboleza kifo cha nyota chipukizi James Kilonzo.
Maelezo ya picha,

Mchezo wa raga nchini Kenya unaomboleza kifo cha nyota chipukizi James Kilonzo.

Mchezo wa raga nchini Kenya unaomboleza kifo cha nyota chipukizi James Kilonzo.

Kilonzo alipigwa risasi alipokuwa akitoa fedha katika mashine ya ATM siku ya Jumatatu katika eneo la makaazi ya Kasarani mjini Nairobi.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alipelekwa hospitalini lakini akatangazwa kufariki baadaye.

Ronny Kangetta ambaye ni meneja wa timu ya raga ya KCB ambapo Kilonzo alikuwa kichezea.

Aliambia Focus Africa kwamba kifo cha Kilonzo ni pigo kubwa.