Greg Rutherford ajiondoa michuano ya dunia mwezi ujao London

Greg Rutherford alishinda medali ya dhahabu Olimpiki 2012
Maelezo ya picha,

Greg Rutherford alishinda medali ya dhahabu Olimpiki 2012

Mrukaji wa viunzi kutoka nchini Uingereza Greg Rutherford amejiondoa katika michuano ya dunia itakayofanyika mwezi ujao mjini London kutokana na kupata maumivu ya kifundo cha mguu.

Rutherford aliyeshinda medali ya dhahabu kwenye mbio za Olyimpiki mjini London mwaka 2012, amesema anasikitika sana kukosa nafasi hiyo muhimu.

Richard Kilty, ambaye alitarajiwa kuchukua nafasi yake nae pia amejiondoa kwa maumivu ya kidole cha mguu.

Lakini But Shara Proctor, Jazmin Sawyers, Lennie Waite, Marc Scott na Jess Turner kwa pamoja wamejumuishwa kwenye kikosi.

Michuano hiyo ya dunia itaanza Agosti 4 mapa 13 mjini London.