Tetesi za soka Ulaya Jumatano 26.07.2017 na Salim Kikeke

Mbappe

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mbappe

Mancheter City wanajaribu kuwapiku Real Madrid katika kumsajili Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Daily Mirror)

Manchester City wapo tayari kutoa pauni milioni 160 kumsajili Kylian Mbappe katika harakati za Pep Guardiola kujenga kikosi chake. (ESPN)

Kylian Mbappe ambaye alipachika mabao 15 katika mechi 29 za Ligue 1 msimu uliopita atakataa kwenda Manchester City akitaka kujiunga na Real Madrid. (Daily Star)

Manchester City hawajapanda dau lolote kumtaka Kylian Mbappe, na wala hawana mpango huo, ingawa Pep Guardiola amesema Real Madrid hawana 'msuli' mkubwa wa kifedha kama wa City. (Sky Sports)

Real Madrid wamefikia makubaliano na Monaco ya kumsajili Kylian Mbappe kwa euro milioni 180. (Marca)

Maelezo ya picha,

Coutinho katikati

Kiungo mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho anakaribia 'sana' kujiunga na Barcelona (Mundo Deportivo)

Barcelona wametuma maafisa wake hapa England kujaribu kumsajili Philippe Coutinho, 25, licha ya Liverpool kukataa dau la pauni milioni 72. (Sports)

Liverpool wanasisitiza kuwa Philippe Coutinho hauzwi, lakini Barcelona wapo tayari kupanda dau la pauni milioni 80. (Daily Star)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema timu yake haiogopi 'kumwaga fedha' msimu huu huku wakiendelea kumsaka beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26. (Daily Mirror)

Liverpool wanatarajiwa kukamilisha usajili wa Virgil van Dijk kutoka Southampton ifikapo mwisho wa dirisha la usajili. (Sky Sports)

Maelezo ya picha,

Mchezaji Thomas Lemar wa Monaco

Arsenal hatimaye wanakaribia kumsajili kiungo wa Monaco Thomas Lemar, 21, kwa pauni milioni 45. (Sun)

Arsenal wanafikiria kumsajili kiungo wa Nice, Jean Michael Seri. (L'Equipe)

Arsenal wanakabiliwa na kupata hasara kwa mshambuliaji wake Lucas Perez, baada ya Deportivo La Coruna kutoa pauni milioni 9 kutaka kumsajili mchezaji huyo, 28. (Evening Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jack Wilshere wa Arsenal anasakwa na West ham

Kiungo wa Arsenal Jack Wilshere, 25, anataka kubakia London iwapo ataondoka Emirates, huku West Ham ikionekana ni kimbilio lake. (Independent)

Stoke City wanataka kununua wachezaji kadhaa katika wiki chache zijazo, lakini hawana mpango wa kumtaka winga wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain, 23. (Stoke Sentinel)

Kiungo wa Bayern Munich Renato Sanches, 19, amesema anataka kuondoka Ujerumani huku AC Milan na Manchester United wakimnyatia mchezaji huyo mwenye thamani ya pauni milioni 43. (Independent)

Maelezo ya picha,

Renato Sanchez

Tottenham wanafikiria kumsajili beki wa Hoffenheim Jeremy Toljan, 22, baada ya mazungumzo ya kumsajili beki Ricardo Pereira, 23, wa Porto kukwama. (Daily Mail)

Everton wamepanda dau la pili la pauni milioni 45 kutaka kumsajili kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson. (The Telegraph)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Uwe na wiki njema.