Monacco yafanya mazungumzo ya kandarasi mpya na Mbappe

Kylian Mbappe

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Kylian Mbappe

Klabu ya Monaco imeanza mazungumzo ya kumuongezea kandarasi mshambuliaji wake Kylian Mbappe kulingana na makamu wa rais wa klabu hiyo Vadim Vaslyev.

Mbappe ambaye ana kandarasi hadi mwezi juni 2019 amehusishwa na uhamisho wa Real Madrid.

Manchester City pia imehusishwa ,lakini BBC Sport inaelewa kwamba hawako tayari kulipa kitita cha Yuro milioni 180 za uhamisho wa mchezaji huo.

Vaslyev alisema kuwa klabu hiyo ya ligue One imepata maombi kuhusu mchezaji huyo.

Lakini ameongezea :Tunazungumza kuhusu kumuongezea kandarasi Kylian na kwamba tuna matumaini yakukubaliana.

Mbappe aliifungia Monaco mabao 26 katika mashindano yote .

Mapema mwezi Julai Monaco ilisema:Vilabu muhimu kutoka Ulaya viliwasiliana na mchezaji huyo bila ruhusa yao.