Manchester City yaicharaza Real Madrid 4-1

Danilo Kushoto

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Danilo Kushoto

Meneja Pep Guardiola amesema Benjamin Mendy atasubiri kwa wiki mbili ama tatu baada ya Manchester City kuicharaza Real Madrid 4-1 mechi ya kirafiki mjini Los Angeles.

Mendy aliyejiunga na City kutoka Monaco hakushirikishwa na atakosa mwanzo wa ligi akiwa na jeraha.

''Hatutaki kufanya hatari kwa sababu anatumia nguvu nyingi'',alisema Guradiola.

Mashabiki takriban 93,000 waliisaidia City kushinda mechi yao ya kwanza ya maandalizi ya msimu ujao kupitia mabao yaliofungwa na Nicolas Otamendi, Raheem Sterling, John Stones na Brahim Diaz.

Kutokuwepo kwa Mendy, Danilo alianzishwa katika uwanja wa Los Angeles huku beki huyo wa kushoto akianzishwa dhidi ya timu yake ya zamani baada ya kusajiliwa kwa pauni milioni 26.5.

''Leo tumeona vile tunavyocheza vizuri'',Guardiola alisema.

''Ni mshindani. Yeye na Kyle walisaidia kutengeneza kiungo chetu cha ulinzi .Waliwasiliana .Tuna furaha sana kuhusu hilo''.