Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 28.07.2017 na Salim Kikeke

Arsenal wanakaribia kukamilisha usajili wa pauni milioni 45 kumchukua kiungo wa Monaco Thomas Lemar, 21. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Monaco wamekataa dau la tatu la Arsenal la pauni milioni 44.7 la kumtaka Thomas Lemar. (L'Equipe)

Maelezo ya picha,

Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema hawezi kutoa hakikisho kuwa Gareth Bale atabakia Bernabeu msimu huu

Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema hawezi kutoa hakikisho kuwa Gareth Bale atabakia Bernabeu msimu huu, huku Manchester United wakimfuatilia. (Mirror)

Monaco watakuwa tayari kumuuza Kylian Mbappe kwa timu itakayokuwa tayari kutoa euro milioni 180. (L'Equipe)

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anapanga kutoa pauni milioni 50 kuwasajili Ross Barkley, 23, kutoka Everton na Alex Oxlade-Chamberlain, 23, kutoka Arsenal. (Sun)

Chelsea wamepanda dau kutaka kumsajili kwa mkopo Renato Sanches, 19, kutoka Bayern Munich. (Daily Telegraph)

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochetitino anataka kumsajili Ross Barkley na kumfanya kuwa kiungo wa kati. (Times)

Maelezo ya picha,

Roma wanajiandaa kupanda dau jipya la pauni milioni 32 kumtaka winga wa kimataifa wa Algeria, Riyad Mahrez, anayechezea Leicester. (Mirror)

Roma wanajiandaa kupanda dau jipya la pauni milioni 32 kumtaka winga wa kimataifa wa Algeria, Riyad Mahrez, anayechezea Leicester. (Mirror)

Liverpool wapo tayari kutoa dau la mwisho la zaidi ya pauni milioni 70 kujaribu kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, 22. (Mirror)

Liverpool wanashikilia msimamo wao kuwa Philippe Coutinho, 25, hauzwi, huku Barcelona wakiendelea kumfuatilia. (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Liverpool wanashikilia msimamo wao kuwa Philippe Coutinho, 25, hauzwi, huku Barcelona wakiendelea kumfuatilia. (ESPN)

Limerpool- kwa shingo upande- wameweka bei ya Philippe Coutinho kuwa ni pauni milioni 133, kama kweli Barcelona wanamtaka mchezaji huyo kutoka Brazil. (Sport)

Meneja wa Inter Milan Luciano Spalletti amesema anataka Ivan Perisic kubakia Italia, ingawa hana uhakika kama ataweza kufanya hivyo huku Manchester United wakiendelea kumfuatilia. (ESPN)

Maelezo ya picha,

Inter Milan wameweka kipaumbele katika kumsajili kiungo wa Bayern Munich, Arturo Vidal, na wanajiandaa kutoa dau la euro milioni 50. (Gazzetta dello Sport)

Inter Milan wameweka kipaumbele katika kumsajili kiungo wa Bayern Munich, Arturo Vidal, na wanajiandaa kutoa dau la euro milioni 50. (Gazzetta dello Sport)

Juventus wanaotafuta kiungo mkabaji sasa wamemgeukia Blaise Matuidi, 30, wa PSG, baada ya kuacha kumfuatilia Nemanja Matic, 28, anayenyatiwa na Manchester United. (Independent)

Mwenyekiti wa AC Milan Marco Fassone amesema klabu yake imezungumza na wakala wa mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa, 28. (Sky Sports)

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzima, 29, anatarajiwa kusaini mkataba mpya hata kama klabu yake itamsajili Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Marca)

Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzima, 29, anatarajiwa kusaini mkataba mpya hata kama klabu yake itamsajili Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Marca)

Mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina Paulo Dybala, 23, anayenyatiwa na Manchester United na Barcelona, hana mipango ya kuondoka Juventus msimu huu. (TalkSport)

Wakala wa mchezaji wa Arsenal Lucas Perez amekwenda London kuzungumzia kurejea kwa mshambuliaji huyo Deoportivo La Coruna. (AS)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfersTetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumaa Kareem.