Los Angeles kuandaa Olimpiki 2028

Carl Lewis Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Carl Lewis

Jimbo la Los Angeles limeteuliwa rasmi kuandaa mashindano ya Olimpiki ya wakati wa majira ya joto mwaka 2028 katika makubaliano yatakayoihakikishia Paris kuandaa Olympiki ya mwaka 2024.

Miji yote miwili ilikuwa akipigania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo makubwa duniani katika tarehe za awali.

Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach amesema anakaribisha uamuzi huo wa Los Angeles kukubali kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa tarehe za mbele.

Kamati hiyo ya Olimpiki imesema itatoa mchango wake wenye thamani ya dola bilioni 0.8 kwa mji wa Los Angeles ili kufidia gharama zitakazoongezeka.