Usain Bolt afananishwa na Muhammed Ali

Usain Bolt afananishwa na aliyekuwa bingwa wa ndondi Muhammed Ali Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Usain Bolt afananishwa na aliyekuwa bingwa wa ndondi Muhammed Ali

Usain Bolt ana kipaji na ana ushawishi mkubwa miongoni mwa wanariadha kama Muhammed Ali alivyokuwa na ushawishi miongoni mwa mabondia, alisema Lord Coe.

BIngwa huyo wa mbio fupi ambaye ameshinda medali ya dhabau katika michezo ya olimpiki mara nane anatarajiwa kustaafu baada ya mashindano ya ubingwa mjini London, yalioanza siku ya Ijumaa.

Coe alimfananisha raia huyo wa jamaica na mmoja wapo wa wanamichezo mashauri duniani Muhammed Ali.

Ni bingwa wa mbio fupi duniani,alisema Coe ambaye ndio raisi wa shirikisho la wanariadha duniani IAAF.

Usain Bolt ana kipaji.Siwezi kumfananisha na mwanamichezo mwengine yeyote yule zaidi ya Muhammad Ali, ambaye amekuwa na ushaiwishi mkubwa nje na ndani ya michezo.

Unaweza kuanzisha mjadala kuhusu ni nani mchezaji bora wa soka duniani ama mchezaji wa tenisi bora, lakini hakuna mjadala kuhusu Bolt katika mbio fupi.

Mwanariadha huyo wa Jamaica alishinda mio za mita100, 200 na 4 by 100 katika michezo iliopita ya Olimpiki mjini Beijing 2008, mjini London 2012 na mjini Rio 2016.

Mada zinazohusiana