Wladmir Klitschko astaafu katika ndondi na kufuta mechi dhidi ya Anhtony Joshua

Wladmir Klitschko astaafu katika ndondi Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wladmir Klitschko astaafu katika ndondi

Aliyekuwa bingwa wa dunia katika ndondi Wladmir Klitschko amestaafu katika ndondi na hivyobasi kufutilia mbali uwezekano wowote wa mechi ya marudiano dhidi ya Anthony Joshua.

Raia huyo wa Ukraine mwenye umri wa miaka 41 alipigwa knockout katika raundi ya 11 na bingwa wa sasa Joshua katika uwanja wa Wembley mnamo mwezi Aprili .

Joshua mwenye umri wa miaka 27 alitumai kwamba Klitschko atashiriki mechi ya marudiano mjini Las Vegas tarehe 11 mwezi Novemba.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Klitschko ambaye ni bingwa mara mbili wa uzani mzito duniani anakamilisha mapigano yake akiwa ameshinda mara 64 na kushindwa mara 5.

Klitschko ambaye ni bingwa mara mbili wa uzani mzito duniani anakamilisha mapigano yake akiwa ameshinda mara 64 na kushindwa mara 5.