Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 05.08.2017 na Salim Kikeke

Serge Aurier akaribia kujiunga na Manchester United Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Serge Aurier akaribia kujiunga na Manchester United

Chelsea wameripotiwa kuwasiliana na Paris Saint-Germain kutaka kumsajili beki Serge Aurier, 24, huku kukiwa na taarifa kuwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast anakaribia kujiunga na Manchester United. (Manchester Evening News)

Inter Milan wanataka kuwapiku Manchester United na Chelsea katika kumsajili beki Serge Aurier wa PSG. (Calciomercato)

Meneja wa Monaco Leonardo Jardim amedokeza kuwa Kylian Mbappe, 18, anayenyatiwa na Real Madrid, Manchester City, Barcelona na Arsenal, huenda akaondoka kabla ya dirisha la usajili kufungwa. (Independent)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Phillipe Coutinho anyatiwa na Barcelona

Philippe Coutinho, 25, ameachwa katika kikosi cha Liverpool kitakachocheza na Athletic Bilbao siku ya Jumamosi kwa sababu ya jeraha la mgongo. Mchezaji huyo ananyatiwa na Barcelona ili kuziba nafasi ya Neymar. (Mirror)

Barcelona wamewasiliana na Borussia Dortmund kuhusu mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa Ousmane Dembele, 20, ili kuchukua nafasi ya Neymar. (Daily Mail)

Ousmane Dembele amesema anakaribisha taarifa za yeye kuhusishwa na kuhamia Barcelona. (Metro)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Barcelona nao wamejiunga katika mbio za kutaka kumsajili winga wa Monaco Thomas Lemar anayenyatiwa na Arsenal. (L'Equipe)

Barcelona nao wamejiunga katika mbio za kutaka kumsajili winga wa Monaco Thomas Lemar anayenyatiwa na Arsenal. (L'Equipe)

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, 32, amekiri kuwa angependa kurejea England, wakati akizungumza mahakamani kwenye kesi yake ya tuhuma za kukwepa kodi nchini Uhispania. (Cadena SER)

Real Madrid watafikiria kumuuza winga Gareth Bale, 28, kwenda Manchester United, lakini ikiwa tu kipa David De Gea atahusishwa katika mkataba huo. (Don Balon)

Image caption Gareth Bale amemuambia mchezaji mwenzake Luka Modric kuwa anataka kurejea England na kujiunga na Manchester United. (Don Balon)

Gareth Bale amemuambia mchezaji mwenzake Luka Modric kuwa anataka kurejea England na kujiunga na Manchester United. (Don Balon)

Paris Saint-Germain baada ya kumsajili Neymar, sasa wanataka kupambana na Arsenal katika kumsajili kiungo wa Nice Jean Michael Seri, 26. (Metro)

Monaco wapo tayari kupanda dau la pauni milioni 45 kumtaka mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28. (Sun)

Meneja wa Chelsea Antonio Conte imeripotiwa yuko tayari kumruhusu beki Andreas Christensen, 21, kwenda Inter Milan ili kubadilishana na winga Antonio Candreva, 30. (Tuttosport)

Image caption Kiungo wa kati wa Leicester Danny Drinkwater

Kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater yuko tayari kuiambia klabu yake kuwa anataka kuondoka na kujiunga na Chelsea. (Mirror)

Chelsea wamekanusha habari kuwa Antonio Conte anamtoa kwa nguvu Diego Costa, 28, Stamford Bridge. (Independent)

AC Milan wanafikiria kumchukua mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Chelsea Radamel Falcao, 31. (Sky Sport Italia)

Image caption Geoffrey Kongodbia, 26

Kiungo wa Inter Milan Geoffrey Kongodbia, 26, anayesakwa na Liverpool na Tottenham, ameomba kuondoka katika klabu yake. (Gazzetta dello Sport)

Everton huenda wakalipa pauni milioni 50 ambayo itavunja rekodi ya klabu ili kumsajili kiungo wa Swansea Gylfi Sigurdsson, 27. (The Times)

Watford wanamtaka beki wa Liverpool Alberto Moreno, 25, baada ya Liverpool kukataa dau la pauni milioni 11 kutoka Napoli. (Liverpool Echo)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumamosi njema.