Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 06.08.2017 na Salim Kikeke

Image caption Dele All (katikati)

Barcelona wanajiandaa kupanda dau kumtaka kiungo wa Tottenham Dele Alli, 21, baada ya kumuuza Neymnar kwa pauni milioni 200. (Sunday Express)

Bayern Munich wapo tayari kutoa pauni milioni 50 kumsajili kiungo wa Tottenham Eric Dier, 21. (Sun on Sunday)

Arsenal, Liverpool, Manchester City na Barcelona wanamtaka kiungo wa Monaco Thomas Lemar, 21. (Sunday Mirror)

Manchester United na Chelsea wanafikiria kumsajili kiungo wa Barcelona Sergi Roberto. (Don Balon)

Chelsea wanaonekana kuwa tayari kupambana vikali na Manchester United katika kumsajili Gareth Bale kutoka Real Madrid. (Sunday Express)

Barcelona wapo tayari kutoa pauni milioni 120 kumsajili kiungo mshambuliaji wa Liverpool Philippe Coutinho. (Star on Sunday)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Philippe Coutinho

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp tayari anapanga kutaka kumsajili Manuel Lanzini kutoka West Ham kuziba pengo la Philippe Coutinho. (Mundo Deportivo)

Antonio Conte amesema hana nguvu zozote za kuzuia Chelsea kumuuza Eden Hazard. (Sunday Mirror)

Barcelona wapo tayari kuwatoa Andre Gomes na Rafinha kama sehemu ya mkataba wa kumsajili Paulo Dybala kutoka Juventus. (Gazzetta dello Sport)

Everton wataamua kumfuatilia mshambuliaji wa Arsenal Danny Welbeck, 26, iwapo watashindwa kumshawishi Olivier Giroud, 30, kuondoka Emirates. (Sunday People)

Meneja wa Everton Ronald Koeman ana matumaini ya kumsajili beki wa zamani wa Arsenal Thomas Vermaelen, 31, kutoka Barcelona. (Sun on Sunday)

Arsenal wanaongoza katika mbio za kutaka kumsajili Lucas Moura kutoka Paris Saint-Germain. (UOL)

Real Madrid wamemhakikishia Gareth Bale, 28, kuwa bado ana nafasi katika klabu hiyo katika hatua ambayo pengine itawahuzunisha Manchester United. (Observer)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gareth Bale

Chelsea wana matumaini ya kuwazidi kete Liverpool katika kumsajili beki wa Southampton Virgil van Dijk, 26. (Evening Standard)

Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri ameiambia Chelsea kuwa "hawana nafasi yoyote" na kumsajili beki kutoka Brazil Alex Sandro, 26. (ESPN)

Swansea lazima walipe pauni milioni 13 ikiwa wanataka kumsajili tena Wilfried Bony kutoka Manchester City. (Sunday Mirror)

Meneja wa Borussia Dortmund Peter Bosz amesema hana wasiwasi kuhusu kumpoteza mshambuliaji wake Ousmane Dembele, 20, anayenyatiwa na Barcelona. (Metro)

Barcelona wanamtaka kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast Jean-Michael Seri, 26, anayechezea Nice, ambaye pia anasakwa na Arsenal. (Mundo Deportivo)

Image caption Jean-Michael Seri

Matumaini ya Liverpool kumsajili kiungo wa Rennes, Benjamin Andre, 27, yamefifia. (Sunday Express)

Newcastle wanamtaka kipa wa West Ham Adrian, 30, ili kuimarisha safu yao ya makipa. (Sky Sports)

Mnunuzi ambaye bado hajafahamika kutoka China ameonesha nia ya kutaka kununua baadhi ya hisa za Manchester United. (Sunday Times)

Usikose kuungana nasi leo moja kwa moja kutoka Wembley kusikiliza mpambano wa Ngao ya Hisani kati ya Arsenal dhidi ya Chelsea. Kuanzia saa kumi alasini saa za Afrika Mashariki.

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumapili njema.