Wenger asema anataka kuanza msimu vyema

Arsenel celebrate Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsenal ikisherehekea

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger, anasema anajiamini kutokana ushindi wa ngao ya jamii dhidi ya Chelsea, na analenga kuzuia kipindi kibaya kwenye mechi za Primia wakati watakutana na Leicester siku ya Ijumaa.

Arsenal wameshindwa wakati wa siku ya kwanza kwenye mechi tatu katika misimu minne iliyopita.

Watakutana na Leister katika uga wa Emirates baada ya kuishinda Chelsea kwa mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare ya bao moja.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsenal

Alexis Sanchez na Mesut Ozil walianza msimu wa mikataba yao mipya lakini wote hawakucheza mechi ya Wembley, lakini wote kujiunga kusherehekea penalti ya ushindi wa Olivier Giroud.

Naye Wenger anasema kuwa ana uhakika kuwa kikosi chake kitakuwa na furaha na kucheza vyema mechi zinazokuja.

Washindi 13 katika 25 wa primia tangu mwaka 1992 wamekuwa ni vilabu ambavyo vimeanza msimu kwa kung'ang'ania mechi ya ngao ya jamii.

Haki miliki ya picha Instagram
Image caption Sanchez hakucheza anaposubiri kupona jeraha

Hata hivyo ni washindi saba ambao wamefanikiwa kushinda kombe huku Manchester ikiwa ya mwisho kafanya hivyo msimu wa mwaka 2010-2011.

Wenger na Meneja wa Chelsea Antonio Conte, wote wanatarajia vilabu vyao kupata ushindi wa primia.