Mourinho: Nitamsajili Gareth Bale akiuzwa

Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale
Image caption Mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa atakabiliana na makocha wengine kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale iwapo Real Madrid wanataka kumuuza.

Bale mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na mabingwa hao wa Uhispania kwa fedha za uhamisho zilizovunja rekodi ya £85m kutoka Tottenham.

Mabingwa wa ligi ya Yuropa Man United wanakutana na Real Madrid ambao walishinda kombe la vilabu bingwa Ulaya katika kombe la Supercup Jumanne.

''Iwapo atashiriki ni ishara tosha kwamba atasalia Madrid'', alisema meneja wa Real Madrid

Mourinho alisema kuwa iwapo Bale atashiriki katika mechi hiyo basi atakuwa katika mpango wa kocha wake na klabu na ni haki na mpango wake kusalia.Basi sitafikiria kumpigania.

''Iwapo hayupo katika mpango wa klabu na ni kweli mchezaji kama Bale anataka kuondoka nitajaribu kuwa hapo nikimsubiri upande mwengine''.

Bale aliimarisha kandarasi yake katika klabu hiyo mwaka uliopita akisema anafurahi kusalia na mabingwa hao mara 12 wa kombe la vilabu bingwa.