Mwanariadha wa Botswana Isaac Makwala akimbia peke yake na kufuzu mbio za mita 200

Huwezi kusikiliza tena
Hata alipiga mazoezi kidogo baada ya kukimbia

Mwanariadha wa Botswana Isaac Makwala atajiunga na mwanariadha wa Afrika Kusini Wayde van Niekerk, katika kuwania ubingwa wa dunia wa fainali ya mita 200 baada ya kukimbia pekee yake na kufuzu huko London jana.

Makwala alikosa kushiriki mbio za siku ya Jumatatu alipozuiwa kushiriki na maafisa, kufuatia mlipuko kwa ugonjwa unaojulikana kama norovirus.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Isaac Makwala

Aliruhusiwa kukimbia hiyo jana ambapo alikimbia muda wa sekunde 20.20 peke yake na kufanikiwa kufuzu.

Mwanariadha raia wa Marekani Isiah Young alishinda nusu fainali ya kwanza kwa sekunde 20.19 huku muingereza Mitchell-Blake akimaliza wa tatu kwa sekunde 20.19

Huwezi kusikiliza tena
Van Niekerk pia alifuzu kwa fainali

Nilikuwa tayari kukimbia mita 400 peke yangu - Makwala

Huwezi kusikiliza tena
Isaac Makwala

Akikimbia katika laini ya kwanza huku mvua ikinyesha ambapo alikimbia kwa muda wa sekunde 20.14 mara ya pili jioni.

"Bado nimevunjika moyo," alisema makwala

" IAAF wangeniruhusu nikimbie mbio za miata 400. Nilikuwa tayari kukimbia mita 400 peke yangu ndio nikimbie mita 200.

"Mbio za mita 400 ndizo ninajifunza.

Awali makwala alikimbia peke yake katika laini ya saba, na kufuzu kwa njia rahisi.

Baada ya kukosa kukimbia mbio za kufuzu za mita 200 na fainalia ya mita 400, IAAF ilimpa Makwala fursa nyingine ya kukimbia mita 200 baada ya kupata barua kutoka kwa shirikisho la riadha la Botswana.

Mada zinazohusiana