Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 11.08.2017 na Salim Kikeke

Alexi Sanchez
Image caption Alexi Sanchez

Arsenal wamempa Alexis Sanchez mkataba mpya na mshahara wa pauni 300,000 kwa wiki na kumfanya mchezaji anayelipwa zaidi katika EPL. (Daily Mail)

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amekiri kuwa "hana uhakika sana" kama ataweza kumshawishi Alexis Sanchez kukubali kusaini mkataba mpya. (SFR)

Juventus wanajiandaa kutoa pauni milioni 23 kujaribu kuishawishi Liverpool kumuuza Emre Can. (Gazzetta dello Sport)

Juventus nao wameingia katika mbio za kutaka kumsajili Sergi Roberto kutoka Barcelona, ambaye pia Manchester United na Chelsea zinamtaka. (Sport.es)

West Ham wamepanda dau la pauni milioni 27.1 kumtaka kiungo wa Sporting Lisbon William Carvalho, 25. (Daily Telegraph)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Liverpool hawataki kumuuza Philippe Coutinho kwa Barcelona

Barcelona hawatakuwa na uwezo wa kumnunua Philippe Coutinho kutoka Liverpool iwapo watafanikiwa kumsajili Ousmane Dembele, 20, kutoka Borussia Dortmund, kwa mujibu wa mwandishi wa ha1ba12ri za michezo Graham Hunter. (BBC Radio 5 Live)

Barcelona wapo tayari kuwapa Liverpool Ivan Rakitic kama sehemu ya mkataba wa kumsajili Philippe Coutinho. (Don Balon)

Barcelona wanamtaka kiungo mchezeshaji wa Real Madrid Marco Asensio na wapo tayari kutoa pauni milioni 72. (Diario Gol)

Mwenyekiti wa Tottenham Daniel Lexy anakabiliwa na sekeseke la wachezaji kudai kuongezewa mishahara baada ya beki Danny Rose kushutumu sera za klabu hiyo. (Daily Mirror)

Danny Rose alipokelewa kwa shangwe na wachezaji wenzake baada ya kuweka wazi mtazamo wa Tottenham, huku wachezaji wengine wakitishia na wao kuweka mambo hadharani. (Daily Mirror)

Wachezaji nyota wa Tottenham wanataka kuondoka kwa sababu ya sera ya malipo ya klabu hiyo. (Daily Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Danny Rose alifunga mabao 18 Ligi ya Premia msimu uliopita

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anatafuta beki wa kushoto na Danny Rose wa Tottenham ni mmoja wa wachezaji anaowafuatilia. (Daily Record)

Meneja wa Everton Ronald Koeman ameiambia Tottenham kuwa hawataweza kumsajili kiungo Ross Barkley kwa bei rahisi. (Daily Star)

Arsenal wanaamini kuwa wamefanikiwa katika mazungumzo ya kumshawishi Mesut Ozil kubakia Emirates baada ya kumpa mkataba wa mshahara wa pauni 225,000 kwa wiki, na mchezaji huyo ameonesha dalili za kukubali. (Sun)

PSG wapo tayari kuwapa Atletico Madrid Javier Pastore katika mkataba wa kumsajili kipa Jan Oblak, 24. (AS)

Real Madrid wamekuwa na mazungumzo ya siri na Juventus kuhusiana na mshambuliaji Paulo Dybala, 23, ambaye pia anasakwa na Barcelona. (Don Balon)

Juventus wanamtaka Kevin Strootman kabla ya dirisha la usajili kufungwa, huku Roma wakisema bei yake ni euro milioni 45. (Tuttosport)

Haki miliki ya picha Getty Images

Arsene Wenger amesema meneja wa Chelsea Antonio Conte awarejeshe wachezaji wanaocheza nje kwa mkopo kama ana wasiwasi na dogo wa kikosi chake. (Times)

Msimu wa EPL unaanza rasmi leo. Arsenal wanacheza na Leicester City saa nne kasorobo usiku huu kwenye uwanja wa Emirates.

Matokeo ya mchezo huo utayapata hapa, bbcswahili.com.

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii (Kwa Kiingereza: Uhamisho wa wachezaji Ulaya

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumaa Kareem.

Mada zinazohusiana