Giroud aiongoza Arsenal kuilaza Leicester

Giroud akishangilia baad ya kufunga bao la ushindi la Arsenal Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Giroud akishangilia baad ya kufunga bao la ushindi la Arsenal

Mchezaji wa ziada Olivier Giroud alifunga kichwa kizuri katika ushindi wa kushangaza baada ya Arsenal kutoka nyuma na kuilaza Leicester katika mechi kali ya ufunguzi wa ligi ya Uingereza.

The Gunners walikuwa nyuma 3-2 huku ikiwa imesalia dakika saba kabla ya Aaron Ramsey na Giroud kuingia na kufunga mabao hayo mawili yalioipatia Arsenal ushindi huo.

Alexandre Lacazette aliiweka kifua mbele Arsenal sekunde 94 baada ya kuanzishwa kabla ya Shinji Okazaki kusawazisha dakika mbili baadaye

.Vardy baadaye aliwaweka mbele wageni hao kufuatia krosi muruwa iliopigwa na Albrighton, kabla ya Danny Welbeck kusawazisha dakika za lala salama katika kipindi cha kwanza.

Leicester ilichukua tena uongozi baada ya Vardy kufunga kona iliopigwa na Mahrez hatua iliomlazimu Wenger kufanya mabadiliko yaliozaa matunda.

Mchezaji wa ziada Ramsey alifunga akiwa karibu na goli kutoka kona iliopigwa na Mesut Ozil kabla ya Giroud kufunga kichwa chengine kupitia kona iliopigwa na Granit Xhaka.