Kiongozi wa zamani wa al-Shabaab ajisalimisha Somalia

Bwana Robo alikuwa naibu kiongozi wa al-Shabaab na msemaji wake kabla ya kutofautiana na kundi hilo miaka minne iliyopita.
Image caption Bwana Robo alikuwa naibu kiongozi wa al-Shabaab na msemaji wake kabla ya kutofautiana na kundi hilo miaka minne iliyopita.

Maafisa nchini Somalia wanasema kuwa mwanachama wa cheo cha juu wa kundi la al-Shabaab Mukhtar Robow amejisalimsha kwa serikali.

Alijisalimisha pamoja na wapiganaji wake katika mji ulio kusini magharibu wa Hudur.

Bwana Robo alikuwa naibu kiongozi wa al-Shabaab na msemaji wake kabla ya kutofautiana na kundi hilo miaka minne iliyopita.

Mwezi Juni, Marekani iliondoa zawadi ya dola milioni tano kwa bwana Robow ambaye bado anaaminiwa kuendelea na shughuli zake kama mwanamgambo.

Al Shabab bado inathibiti maeneo makubwa ya Somalia na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara nchini Kenya.

Mada zinazohusiana