Ronaldo apigwa marufuku ya mechi tano

Ronaldo baada ya kupewa kadi nyekundu Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ronaldo baada ya kupewa kadi nyekundu

Mchezaji nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amepewa marufuku ya mechi tano baada kupewa kadi nyekundi wakati wa mechi ya el Clasicco siku ya Jumapili.

Alipewa marufuku ya mechi moja kwa kuonyeshwa kandi mbili za njano na nyengine nne kwa kumsukuma refa kutoka nyuma baada ya kutolewa nje.

Alipewa kadi nyekundu kwa kuvua tishati yake alipokuwa akisherehekea bao lake lililofanya mambo kuwa 2-1 na kujirusha

Atakosa mechi ya Jumatano ya awamu ya pili.

Ronaldo ana siku 10 kukata rufaa.

Raia huyo wa Ureno atacheza katika ligi ya mabingwa lakini hatocheza hadi tarehe 20 mwezi Septemba dhidi ya Real Betis.

Madrid tayari ilikuwa ishatoa ishara za kutaka kukata rufaa dhidi ya kadi ya pili ya njano dakika nane kabla ya mchezo kukamilika alipojiangusha ndani ya eneo hatari baada ya kubanwa na Samuel Umtiti.