Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 19.08.2017 na Salim Kikeke

Haki miliki ya picha PA
Image caption Philippe Coutinho

Dau la Barcelona la Pauni milioni 119 la kumtaka Philippe Coutinho limekataliwa na Liverpool. Barca walikuwa tayari kutoa pauni milioni 80, na kiasi kilichosalia kama nyongeza iwapo Coutinho atashinda Ballon d'Or na makombe mengine. (Mirror)

Barcelona watamgeukia Jean Michel Seri iwapo watashindwa kumsajili Philippe Coutinho, 25, kutoka Liverpool. (SPORT)

Barcelona wanakaribia kukamilisha usajili wa winga wa Paris Saint-Germain Angel Di Maria. (The Sun)

Monaco wamesema bei ya Kylian Mbappe ni euro milioni 200, huku PSG wakiendelea kumnyatia. (Sky Sport)

Paris Saint-Germain watatangaza usajili wa Kylian Mbappe, 19, kutoka Monaco, kwa euro milioni 180 na kuwa mchezaji wa pili aghali zaidi duniani nyuma ya Neymar. (Mundo Deportivo)

Chelsea wanataka pauni milioni 50 kumuuza Diego Costa, 28, lakini Atletico Madrid wako tayari kutoa pauni milioni 30. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Diego Costa

Dau la pauni milioni 63 la Chelsea kumtaka mshambuliaji wa Torino Andrea Belotti limekataliwa. (The Sun)

Chelsea wanamtaka winga wa Inter Milan Antonio Candreva, 30, huku Milan wakiwa tayari kumuuza kwa pauni milioni 25. (Mirror)

Real Madrid wanapanga kupanda dau la pauni milioni 46 kumtaka kipa wa Manchester United David de Gea. (The Sun)

Manchester United watamruhusu kipa David de Gea, 26, kujiunga na Real Madrid msimu ujao iwapo wataweza kumsajili kipa wa AC Milan Gianluigi, 18, Donnarumma. (Sun)

West Ham wanaghadhibishwa na jitihada za kutaka kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon William Carvalho, 25, huku timu hizo mbili zikivutana kuhusu tofauti ya pauni milioni 5.5 katika bei ya usajili. (Telegraph)

Manchester City wameambiwa lazima walipe takriban pauni milioni 30 ikiwa wanataka kumsajili beki wa West Brom, Jonny Evans, 29. (Times)

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Jonny Evans

Paris Saint-German wamesema hawatopokea dau lolote msimu huu la kumuuza winga Julian Draxler, 23. (ESPN)

Inter Milan wameonesha nia ya kutaka kumsajili kwa mkopo beki wa Arsenal Shkodran Mustafi. (GianlucaDiMarzio.com)

Licha ya Arsenal kumnyatia, Marco Asensio, mchezaji huyo anajiandaa kusaini mkataba mpya wa kubakia Real Madrid hadi mwaka 2023 na pia kusaini kipengele cha uhamisho chenye thamani ya euro milioni 500. (Marca)

Arsenal wapo tayari kupanda dau kumtaka winga wa PSG Julian Draxler msimu huu, huku PSG wakitaka pauni milioni 32. (The Times)

Real Madrid wamekataa dau la fedha nyingi kutoka kwa Juventus kumtaka Mateo Kovacic. (AS)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mateo Kovaci

Tottenham wapo katika mazungumzo ya kina kutaka kumsajili beki wa kati wa kimataifa wa Argentina Juan Foythe, 19, anayechezea Estudiantes, kwa pauni milioni 9. (Guardian)

Kiungo mpya wa Everton Gylfi Sigurdsson, 27, amesema hana majuto yoyote kuhusiana na mtafaruku uliozuka wakati wa mchakati wa uhamisho wake wa pauni milioni 40 kutoka Swansea. (Times)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumamosi njema.