Manchester United yainyoa Swansea bila maji yainyuka mabao 4-0

Paul Pogba (left) and Eric Bailly both scored for Manchester United Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Paul Pogba (kushoto) na Eric Bailly wote waliifungia Manchester United

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho, anasema kuwa "aliachia farasi kukimbia watakavyo," baada ya kikosi chake kuinyeshea magoli 4-0 Swansea na kuanza msimu kwa ushindi.

"Kulikuwa na furaha kwenye mchezo wetu, alisema Mourinho.

"Nilihisi kudhibiti hali, kama ulikuwa na wakati kuweza kunitazama mimi na mwili wangu, nafikiri ungeona."

Baada ya kuwa na wakati mgumu kuvunja safu ya nyuma ya Swansea, United walifanikiwa kufungua mlango baada ya dakika 80, wakati Romelu Lukaku alifunga bao lake la tatu kwenye mechi mbili.

"Swansea walitumia wachezaji watano nyuma na wakafika kipindi walijua wangefanya mabadiliko, na wakati walaifanya hivyo, tukawa na nafasi zaidi tukacheza vizuri." aliongeza Mourinho.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Martial aliifungua United bao na nne

Mada zinazohusiana