Mchezaji Nicolai Muller aumia akisherehekea kufunga bao

Nicolai Muller Haki miliki ya picha Getty Images

Winga wa klabu ya Hamburg ya Ujerumani Nicolai Muller hataweza kucheza kwa miezi saba ijayo baada yake kuumia kwenye goti akisherehekea kufunga bao.

Baada ya kufunga bao pekee katika mechi dhidi ya Augsburg dakika ya nane siku ya Jumamosi, Muller aliruka ruka na kuzunguka hewani akisherehekea.

Alianguka vibaya na alionekana kuhisi uchungu sana kabla ya wachezaji wenzake kukimbia kuungana naye.

Mkufunzi wa Hamburg Markus Gisdol amesema kilikuwa kisa cha kushangaza.

Mchezaji huyo aliumia kano za goti la kulia na klabu hiyo imesema anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa dakika saba.

Mkurugenzi wa michezo wa kalbu hiyo Jens Todt amesema: "Uchunguzi wa jeraha lake ulitushangaza, ni pigo kubwa sana kwetu mwanzo wa msimu na bila shaka pigo kubwa zaidi kwa Nicolai.

"twamtakia apone haraka na tutamsaidia kadiri ya uwezo wetu."

Muller, 29, alijiunga na Hamburg kutoka Mainz mwaka 2014 na amechezea timu ya taifa ya Ujerumani mara mbili, karibuni zaidi ikiwa mwaka 2013.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nicolai Muller has played twice for Germany, and joined Hamburg in 2014

Mada zinazohusiana