Burnley wavunja rekodi yao ya usajili kumnunua Chris Wood

Chris Wood Haki miliki ya picha Burnley FC
Image caption Chris Wood, alifunga mabao mengi zaidi ligi ya daraja la pili msimu uliopita

Burnley wamemnunua mshambuliaji Chris Wood kutoka Leeds United kwa bei iliyovunja rekodi ya klabu hiyo, ambayo inaaminika kuwa takriban £15m .

Mchezaji huyo wa miaka 25 alifunga mabao 44 katika mechi 88 tangu alipojiunga na Leeds kutoka Leicester City Julai 2015.

Raia huyo waNew Zealand alijiondoa kutoka kwa mechi ya Leeds dhidi ya Sunderland katika ligi ya daraja la pili Jumamosi uvumi kuhusu kuhama kwake ulipokuwa umesheheni.

Wood, ndiye mchezaji wa sita kununuliwa na Sean Dyche kipindi hiki.

Ametia saini mkataba wa miaka minne.

Mchezaji huyo alikuwa amefunga bao moja katika mechi tatu alizowachezea Leeds msimu huu, lakini sasa ataanza kujaribu kutikisa nyavu Ligi ya Premia.

Wood anaruhusiwa kuchezea Burnley katika Kombe la EFL kwani alikuwa benchi na hakuchezeshwa mechi waliyolaza Port Vale.

Rekodi ya awali ya usajili wa Robbie Brady waliyemnunua Januari kwa ada inayotarajiwa kufikia £13m.

Mada zinazohusiana