Alphonce Simbu: Nina matumaini nitaishindia Tanzania dhahabu karibuni

Alphonce Simbu: Nina matumaini nitaishindia Tanzania dhahabu karibuni

Mwanariadha wa mbio za masafa marefu Alphonce Simbu aliweka tena Tanzania kwenye ramani ya dunia baada ya kumaliza wa tatu katika mbio za marathon mashindano ya ubingwa wa dunia London.

Alikuwa awali ameshinda mbio Mumbai.

Simbu anasema lengo lake sasa ni kuangazia kushinda dhahabu katika mashindano makubwa ya dunia.