Man United yailaza Leicester na kusalia kileleni mwa ligi

Man United yailaza Leicester na kusalia kileleni mwa ligi Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Man United yailaza Leicester na kusalia kileleni mwa ligi

Mchezaji wa ziada Marcus Rashford na Marouane Fellaini walifunga bao kila mmoja na kuisadia man United kuilaza Leicester na hivyobasi kuendelea kuoongoza ligi ya Uingereza.

Kikosi hicho cha Jose Mourinho kiliiwekea shinikizo Leicester tangu mechi ianze na Romelu Lukaku alikosa mkwaju wa penalti kabla ya mabao hayo baada ya kushindwa kuvunja ngome ya Foxes.

Nadhani tuliwasumbua kipindi kirefu cha mchezo , alisema Mkufunzi wa Leicester Craig Shakespeare.

Hatahivyo walifanikiwa baada ya rashford kufunga bao kutokana na kona iliopigwa na Henrikh Mkhitaryan dakika tatu baada ya kuingia kama mchezaji wa ziada.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kocha Jose Mourinho

Na baadaye kiungo wa kati Fellaini alifunga krosi iliopigwa na Jesse Lingard.

United ndio timu ya pekee kuwahi kushinda mechi zake tatu msimu huu na bado hawajafungwa.