Tetesi za soka Ulaya Jumapili 27.08.2017 na Salim Kikeke

Liverpool wameweka makataa ya hadi Jumatatu, kwa Barcelona wawe wamefikia bei ya Philippe Coutinho, 25. (Onda Cero)
Image caption Liverpool wameweka makataa ya hadi Jumatatu, kwa Barcelona wawe wamefikia bei ya Philippe Coutinho, 25. (Onda Cero)

Liverpool wameweka makataa ya hadi Jumatatu, kwa Barcelona wawe wamefikia bei ya Philippe Coutinho, 25. (Onda Cero)

Liverpool wanataka kukamilisha usajili wa Alex Oxlade Chamberlain, 24, kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Chelsea pia wanamtaka winga huyo wa Arsenal. (Sunday Mirror)

Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28, imeripotiwa anaitaka klabu yake kumfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi katika EPL iwapo wanataka asaini mkataba mpya. (Daily Star)

Image caption Meneja wa Arsenal Arsene Wenger hajakata tamaa ya kumsajili Thomas Lemar wa Monaco

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger hajakata tamaa ya kumsajili Thomas Lemar wa Monaco, 22, pamoja na Virgil van Dijk, 26, ingawa huenda ikawa msimu ujao. (Sun)

Arsenal wanataka kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Marco Asensio, 21. (Sunday Express)

Paris Saint-Germain wanaendelea na majadiliano ya kumsajili mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe kwa pauni milioni 166 kabla ya dirisha la usajili kufungwa, ingawa Monaco wenyewe wanataka Mbappe aende Real Madrid. (Sunday Telegraph)

Image caption Paris Saint-Germain wanaendelea na majadiliano ya kumsajili mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe kwa pauni milioni 166 kabla ya dirisha la usajili kufungwa

Iwapo Kylian Mbappe ataondoka Monaco, klabu hiyo itataka kuziba pengo lake na Islam Slimani, 29, wa Leicester City. (Leicester Mercury)

Kiungo wa Bayern Munich Renato Sanchez, 20, ameomba kuachwa kwenye kikosi dhidi ya Werder Bremen ili ashughulikie mustakbali wake huku Chelsea na Liverpool zikimfuatilia. (Metro)

Everton wanataka kuwapiku Chelsea katika kumsajili mshambuliaji wa Leicester Jamie Vardy, kwa pauni milioni 40. (Sunday Mirror)

Image caption Tottenham huenda wakataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi, 22, iwapo Vincent Janssen ataondoka. (Sun)

Tottenham huenda wakataka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi, 22, iwapo Vincent Janssen ataondoka. (Sun)

Juventus wanataka kumsajili kiungo wa Barcelona Andre Gomes, 24. (Marca)

Mmiliki wa Valencia amewasili mjini Manchester kuanza mazungumzo ya kumsajili kiungo wa Manchester United Andreas Pereira, 21. (Sunday Express)

Leicester City wanataka kumsajili beki wa Manchester United Chris Smalling. (Daily Mirror)

Image caption Beki wa PSG Serge Aurier anasubiri kibali cha kufanya kazi Uingereza baada ya kukamilisha vipimo vya afya ili kujiunga na Tottenham. (Sky Sports)

Beki wa PSG Serge Aurier anasubiri kibali cha kufanya kazi Uingereza baada ya kukamilisha vipimo vya afya ili kujiunga na Tottenham. (Sky Sports)

Habari zilizothibitishwa tutakujuza mara zitakapothibitishwa. Kwa orodha kamili ya wachezaji waliokamilisha rasmi usajili bofya link hii: http://www.bbc.co.uk/sport/football/transfers

Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Jumapili njema.

Mada zinazohusiana