Liverpool kumenyana na Arsenal ugani Anfield

Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez kulia anaweza kuanza mechi yake ya kwanza msimu huu baada ya kupona jeraha la tumboni. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez kulia anaweza kuanza mechi yake ya kwanza msimu huu baada ya kupona jeraha la tumboni.

Liverpool itamkagua Trent Alexander-Arnold, ambaye alilazimishwa kutoka nje katika mechi dhidi ya Hoffenheim baada ya kupata jeraha la mguu pamoja na Emre Can ambaye alipata jeraha la goti.

Mchezaji Phillipe Coutinho ambaye haijabainika iwapo atasalia katika kikosi cha Liverpool , Adam Lallana na Nathaniel Clyne bado watasalia katika orodha ya majereha.

Mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez anaweza kuanza mechi yake ya kwanza msimu huu baada ya kupona jeraha la tumboni.

Beki wa kati Laurent Kolscieny pia anarudi baada ya kuhudumia marufuku ya mechi tatu.