Conor McGregor: Refa alifanya makosa kusimamisha pigano

Conor McGregor amesema kuwa refa Robert Byrd alifanya makosa kusimamisha pigano
Maelezo ya picha,

Conor McGregor amesema kuwa refa Robert Byrd alifanya makosa kusimamisha pigano

Conor McGregor sasa anasema kuwa refa Robert Byrd alifanya makosa kusimamisha pigano lake dhidi ya Floyd Mayweather katika raundi ya kumi.

Bingwa huyo wa UFC alipigwa katika pigano lake la kwanza la kulipwa huku Floyd Mayweather akiimarisha rekodi yake ya kutoshindwa hadi 50-0.

Raia huyo wa Ireland ambaye amesema atarudi kuendelea na mchezo wake wa UFC licha ya kusema huenda akarudi tena katika ulingo wa ndondi anasema kuwa alikuwa amechoka kiasi.

''Nilidhani pigano hili lilikaribia kuwa sawa, niliyumba yumba kiasi nilipochoka'',alisema.

''Refa angewacha pigano liendelee na kumruhusu Mayweather kuniangusha'' .

''Nilikuwa najua nilichokuwa nikifanya.raundi mbili za mwisho nilitaka nione kama anaweza kuniangusha.Nilidhani ilikuwa mapema mno kwa refa kusimamisha pigano hilo.Nilitaka kuendelea hadi raundi ya mwisho'', alisema.