Lewis Hamilton ashinda Belgian Grand Prix.

ulaya Haki miliki ya picha EPA
Image caption Lewis Hailton

Dereva wa timu ya Mercedes Mwingereza, Lewis Hamilton, ameibuka mshindi katika mbio za Belgian Grand Prix.

Hamilton alitumia muda wa saa moja dakika 24 na sekunde 42 na kuongoz akwa alama 25 dhidi ya wapinzania wake.

Dereva wa timu ya Ferrari, Sebastian Vettel, alishika nafasi ya pili kwa kupata alama 18 huku Daniel Ricciardo, toka timu ya Red Bull, akimaliza katika nafasi ya tatu kwa kupata alama 15.

Dereva mwingine wa Ferrari, Kimi Raikkonen, alimaliza mashindano hayo akiwa nafasi ya nne na Valtteri Viktor Bottas wa Mercedes alishika nafasi ya tano.