Bingwa mpya wa Scrabble duniani atawazwa baada ya kuandika 'carrels'

David Eldar Haki miliki ya picha Andy Paradise/Mattel
Image caption David Eldar alijishindia £7,000

Bingwa mpya wa mchezo wa kuunda maneno kwa kutumia herufi maarufu kama Scrabble ametawazwa baada ya kusaidiwa na ufahamu wake kuhusu samani.

David Eldar, 27, alishinda taji hilo baada ya kuandika "carrels" - aina ya chumba kidogo chenye meza, sana ambavyo hupatikana kwenye maktaba katika vyuo vikuu kumuwezesha mtu kusoma vitabu akiwa faraghani.

Neno hilo lilimzolea Eldar alama 74.

Eldar alimshinda mpinzani wake Harshan Lamabadusurilya 3-0 katika fainali iliyokuwa na michuano mitano.

Tuzo ya Eldar ilikuwa pamoja na hundi ya £7,000.

Mzaliwa huyo wa Australia aliwashinda wapinzani wengine kutoka mataifa 26 yakiwemo Pakistan na Sierra Leone, kushinda taji hilo katika mashindano hayo yaliyoandaliwa Nottingham nchini Uingereza.

Mshindi huo anasema amekuwa akicheza mchezo huo kwa miaka 14 sasa na hufanya kazi katika biashara na uuzaji na ukodishaji wa nyumba na vipande vya ardhi jijini London.

Haki miliki ya picha Andy Paradise/Mattel
Image caption Mashindano hayo yalifanyika kwa siku tatu

"Hii ina maana kubwa sana kwangu," alisema baada ya kushinda.

Lamabadusurilya aliyemaliza wa pili ameorodheshwa nambari 16 duniani na alikuwa amecheza mchezo huo kwa miongo miwili.

Alijishindia £3,000.

Kwenye fainali hiyo, wachezaji waliandika maneno kama vile "obvs," neno la mtaani lenye maana ya "obvious" na kushinda alama kumi, na pia "asinicos," maana yake mtu mjinga, na kujishindia alama 64.

Haki miliki ya picha Andy Paradise/Mattel
Image caption Eldar anasema kuwa makini kwake kulimsaidia

Mada zinazohusiana