Alex Oxlade-Chamberlain kujiunga na Chelsea

Nyota wa Arsenal Alex Oxlaide Chamberlain yuko katika harakati za kujiunga na Chelsea. Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nyota wa Arsenal Alex Oxlaide Chamberlain yuko katika harakati za kujiunga na Chelsea.

Nyota wa Arsenal Alex Oxlade Chamberlain yuko katika harakati za kujiunga na Chelsea.

Chamberlain mwenye umri wa miaka 24 atamaliza mkataba wake msimu ujao na Arsenal na amekataa kuongeza mkataba mpya.

Chelsea imekataa kutoa tamko lolote kuhusu hatua hiyo lakini inadaiwa kwamba tayari wamekubaliana kuhusu fedha za uhamisho huo na wapinzani wao ili kumsajili mchezaji huyo wa Uingereza.

Liverpool pia walikuwa wakimtaka mchezaji huyo na bado wanaweza kuwasilisha ombi la kuvutia ili kumnyakua mchezaji huyo.

Oxlade Chamberlain amecheza kila mechi ya Arsenal kufikia sasa msimu huu ikiwemo kichapo cha 4-0 ilichopata Arsenal dhidi ya Liverpool wakati alipotolewa.

Kiungo huyo wa kati atakuwa mchezaji wa 5 wa Chelsea kusajiliwa kufuatia kuwasili kwa Alvaro Morata, kipa Willy Caballero, beki Antonio Rudiger na kiungo wa kati Tiemou Bakayoko.

Mada zinazohusiana