Ian Wright: Wenger anafaa kuondoka Arsenal

Ian Wright asema kuwa Wenger anafaa kuondoka Arsenal Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ian Wright asema kuwa Wenger anafaa kuondoka Arsenal

Arsenal iko katika hali mbaya ''kuanzia juu hadi chini'' na mkufunzi Arsene Wenger anafaa kuondoka kulingana na aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo Ian Wright.

Kichapo cha 4-0 dhidi ya Liverpool siku ya Jumapili kiliiwacha timu hiyo na ushindi mmoja pekee kati ya mechi zake za kwanza tatu za ligi.

''Ni ndoto mbaya'', alisema Ian Wright ambaye aliifungia Arsenal mabao 128.

''Kwa nini tusipate wachezaji wanaoweza kuichezea Arsenal'',? ''Wenger ndio wa kulaumiwa'', aliambia BBC.

Wright ambaye alikuwa mmoja wa wachezaji wa kikosi cha Wenger walioshinda kombe la FA mara mbili 1997-98 aliongezea: Matatizo yanamrudia mwenyewe.

''Tumecheza mechi tatu na tuko mashakani tayari.Je anafaa kwenda? ndio ningependelea aondoke kwa sababu sidhani kwamba anaweza kuwapatia motisha wachezaji''.

''Ni kwa manufaa na heshima yake mwenyewe''.Ni ndoto kubwa sana -kwa sababu ataelekea wapi baada ya hapa''.

''Timu hii haijamchezea Wenger kwa miaka mingi''.

Wright pia alishangazwa na ripoti kwamba Arsenal imekubali ombi la Chelsea kumsajili Alex Oxlaide-Chamberlain huku akisema kuwa Alexis Sanchez anafaa kuuzwa kabla ya dirisha la uhamisho kumalizika siku ya Alhamisi.

Mada zinazohusiana