Barcelona yamsajili Ousmane Dembele kwa £135.5m

Ousmanne Dembele Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ousmanne Dembele

Barcelona wamekamilisha usajili wa mshambualiji wa Borrusia Dortmund Ousmane Dembele kwa uhamisho wa kitita cha £135.5m.

Mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20 ametia saini kandarasi ya miaka mitano katika uwanja wa Nou Camp akiwa na rais wa klabu hiyo Josep Maria Bartomeu siku ya jumatatu.

Kandarasi hiyo ni ya pili kwa thamani baada ya ile ya hivi karibuni ya Neymar kuelekea PSG iliogharimu pauni milioni 200.

Dembele: Nafurahia sana kujiunga na Barca .

''Imekuwa ndoto yangu tangu nikiwa mdogo kuichezea Barca na sasa nimewasili''.

''Ndio klabu bora duniani ilio na wachezaji bora duniani''.

Mara ya mwisho kwa Dembele kuichezea Dortmund ni wakati wa kombe la Supercup mnamo tarehe 5 mwezi Agosti.

Klabu hiyo ya Bundesliga ilikataa ombi la Barca mapema mwezi Agosti , huku mchezaji huyo akiwa amepewa marufuku kwa kukosa mazoezi.

Mada zinazohusiana