Ajuza wanaocheza ndondi Afrika Kusini

Ajuza wanaocheza ndondi Afrika Kusini

Ndondi ni mchezo mgumu ambao bila shaka huwezi kuuhusisha na wazee.

Lakini katika mtaa wa Cosmo City nchini Afrika Kusini, katika kituo kimoja cha mazoezi, utashangaa kuwapata ajuza wakipokea mafunzo.

Wanasema wanatumia mchezo huo wa ndondi kuimarisha miili na afya yao, na pia wanaweza kuutumia kujilinda.